Wang Yi kushiriki mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje wa kundi la nchi 20
2021-06-29 09:21:26| cri

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Bw. Wang Yi leo anatarajiwa kushiriki kwenye mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje wa kundi la nchi 20 unaofanyika kwa njia ya video.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Bw. Wang Wenbin leo hapa Beijing amesema China itatumia mkutano huo kuhimiza pande mbalimbali kutetea moyo wa wenzi, kuimarisha mshikamano na ushirikiano, kutoa ishara yenye nguvu kwa nje katika kuongoza mapambano dhidi ya virusi vya Corona, kufufua uchumi wa dunia, kukamilisha usimamizi wa uchumi duniani, na kutafuta maendeleo endelevu na shirikishi, ili kuweka msingi kwa mafanikio ya mkutano wa kilele wa Roma na kuingiza imani na uhai kwa dunia kushinda virusi hivyo na kufanya uchumi ufufuke kwa utulivu.