Marais wa China na Russia watangaza kurefusha mkataba wa ushirikiano wa kirafiki kati ya nchi zao
2021-06-29 09:03:43| CRI

Rais Xi Jinping wa China na mwenzake wa Russia Vladimir Putin wametoa taarifa ya pamoja wakiamua kurefusha rasmi mkataba wa ujirani mwema na urafiki kati ya nchi zao.

Tangazo hilo limekuja wakati wa mazungumzo yaliyofanyika kwa njia ya video kati ya viongozi hao.

Akipongeza maadhimisho ya miaka 20 ya kusainiwa kwa mkataba huo wa urafiki, Rais Xi amesema mkataba huo ulianzisha urafiki wa muda mrefu, unaoendana na maslahi ya kimsingi ya nchi hizo mbili, na amani na maendeleo, na kuwa mfano hai wa kujenga ushirikiano mpya wa kimataifa na kujenga jumuiya ya binadamu yenye mustakbali wa pamoja.

Rais Putin amesema mkataba huo inaonyesha urafiki wa kudumu wa watu wa nchi hizo mbili, na Russia inaridhika na kiwango cha juu cha urafiki kati ya China na Russia. Pia amesema kurefushwa kwa mkataba huo kutaweka msingi imara zaidi kwa maendeleo ya muda mrefu ya ushirikiano kati ya pande hizo mbili.