Rais Xi Jinping: Wanachama wa CPC wana imani thabiti
2021-06-29 11:12:24| CRI

Rais Xi Jinping wa China amesema washinda nishani ya Julai Mosi wameonesha wazi kuwa wanachama wa CPC wana maadili yenye imani thabiti, kutumikia malengo ya chama, moyo wa kujitolea, bidii na uadilifu. Amewataka wanachama wote waichukulie imani kwa nadharia ya Umaksi na Ujamaa wenye umaalumu wa China kuwa lengo wanalofuata katika maisha yao yote.

Rais Xi Jinping amesema hayo alipohutubia hafla ya kutunuku nishani ya Julai Mosi iliyofanyika leo mjini Beijing. Amesema katika miaka zaidi ya mia moja iliyopita, wanachama wa CPC wa kizazi kimoja baada ya kingine wamejitolea kwa damu na jasho kwenye shughuli kubwa za kupigania uhuru wa taifa, ukombozi wa watu na kutimiza ustawishwaji wa nchi na uboreshwaji wa maisha ya watu. Kila mwanachama anatakiwa kukumbuka moyoni lengo la asili la chama.