Vyombo vya habari vya kigeni vyasema utawala wa CPC waboresha maisha ya Wachina
2021-06-30 10:44:13| CRI

 

 

Vyombo vya habari vya kigeni vikiwemo vya nchi za magharibi hivi karibu vimesema, sababu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) kupata mafanikio makubwa katika kukuza uchumi ni kuungwa mkono sana na wananchi wa China.

Gazeti la Yomiuri Shinbun la Japan limesema, chini ya uongozi wa CPC, uchumi wa China umekua kwa kasi ya kushangaza, na sasa China imekuwa nchi ya pili kwa nguvu ya uchumi duniani.

Tovuti ya habari ya Business Insider ya Marekani imesema, mfumo wa kisiasa wa China unahakikisha Wachina wengi wananufaika na maendeleo ya uchumi.

Gazeti la LeMonde la Ufaransa limesema Chama cha Kikomunisti cha China kinajua lini na jinsi kinavyopaswa kufanya mageuzi kuendana na zama husika.

Gazeti la The Economist limesema, Wachina waliozaliwa baada ya mwaka wa 1990 wanapenda utamaduni na bidhaa za kisasa za nchi za nje, lakini pia wanaona fahari kwa utamaduni na mafanikio yaliyopatikana nchini China.