WHO imethibitisha kuwa China imetokomeza Malaria baada ya juhudi za miaka 70
2021-06-30 09:13:23| cri

Shirika la Afya Duniani WHO limeitangaza China kuwa nchi iliyotokomeza ugonjwa wa Malaria.

Taarifa iliyotolewa na WHO inasema Mkurugenzi wa Shirika hilo Bw. Tedros Ghebreyesus ameipongeza China kwa mafanikio hayo, na kusema yamepatikana kutokana na kazi ngumu na ya muda mrefu.

Amesema kutokana na taarifa hiyo, China imeungana na nchi nyingine duniani na kuionyesha dunia kuwa, siku za baadaye zisizo na malaria zinawezekana.