Ofisi ya Habari ya Baraza la Serikali ya China yatoa Waraka Mweupe wa “Mfumo wa Aina Mpya ya Vyama vya Kisiasa vya China”
2021-06-30 15:22:47| CRI

Shirika la Habari la China Xinhua Juni 25 lilitoa habari zikisema kuwa, Ofisi ya Habari ya Baraza la Serikali ya China tarehe 25 ilitoa waraka mweupe wa “Mfumo wa Aina Mpya ya Vyama Kisiasa vya China”.

Mfumo wa vyama vya kisias ni muundo muhimu wa kutimiza siasa ya kidemokrasia katika zama za hivi sasa, na ni sehemu muhimu ya mfumo wa siasa ya nchi. Nchi moja inafuata mfumo wa namna gani wa vyama vya kisiasa, hii inaamuliwa na mila na desturi za historia na hali halisi ya nchi hiyo. Mifumo ya vyama vya kisiasa ya nchi mbalimbali duniani ni ya aina mbalimbali, lakini hakuna mfumo wa aina moja ambao unaweza kuzifaa nchi nyingi, tena haiwezekani kuwepo kwa mfumo kama huo. Mfumo wa ushirikiano wa vyama mbalimbali na mashauriano ya kisiasa chini ya uongozi wa Chama cha kikomunisti cha China ni mfumo wa kisiasa wa kimsingi wa China.  

Mfumo huu umekita mizizi kwenye ardhi ya China na kuonesha wazi busara za China, pia umeingia na kupata matunda bora ya ustaarabu wa kisiasa wa binadamu, nao ni mfumo wa aina mpya wa vyama vya kisiasa. Katiba ya Jamhuri ya Watu wa China ina kifungu kikisema: “Mfumo wa ushirikiano wa vyama mbalimbali na mashauriano ya kisiasa chini ya uongozi wa Chama cha Kikomunisti cha China utakuwepo na kukua kwa muda mrefu.”

Mfumo huo wa aina mpya umehusisha Chama cha Kikomunisti cha China na vyama vinane vya kidemokrasia, pamoja na watu wasio na chama. Vyama vinane vya kidemokrasia vikiwemo pamoja na Kamati ya Mapinduzi ya Chama cha Koumintang cha China, Muungano wa Kidemokrasia wa China, Shirikisho la Kujenga nchi kidemokrasia la China, Shirikisho la Uhimizaji wa Demokrasia la China, Chama cha Kidemokrasia cha wakulima na wafanyakazi cha China, Chama cha Zhi Gong, Shirikisho la Wasomi la Jiu San, na Muungano wa Kujiendesha kidemokrasia wa Taiwan. Chama cha Kikomunisti cha China kinakuwepo pamoja na vyama mbalimbali vya kidemokrasia siku zote, ambapo vinasimamiana, vinatendeana kwa udhati, na vinakuwa pamoja katika dhiki na faraja, na ukaundwa muundo wa kisiasa wa “Chama cha Kikomunisti kinaongoza, vyama vingi vinashirikiana, Chama cha Kikikomunisti kinafanya utawala wa nchi, na vyama mbalimbali vinashiriki kwenye mambo ya kisiasa”.

Mfumo wa aina mpya wa vyama vya kisiasa wa China umevumbua mfumo wa aina mpya wa siasa ya vyama, mfumo huu umeonesha ubora peke yake na nguvu kubwa ya uhai katika maisha ya kisiasa na kijamii nchini China, na umeonesha umuhimu wake usio na mbadala wake katika kusukuma mbele ujenzi wa mambo ya kisasa wa mfumo wa utawala wa nchi na uwezo wa kutawala nchi, pia umetoa mchango mkubwa kwa ajili ya maendeleo ya ustaarabu wa kisiasa wa binadamu.

Vyama mbalimbali vya kidemokrasia nchini China vilianzishwa na kukua katika mapambano ya Watu wa China ya kupinga ubeberu na kupenda nchi, kujipatia demokrasia na kupinga udikteta, msingi wake wa jamii ni tabaka la mabwanyenye wazalendo, tabala la mabwanyenye wadogo mijini pamoja na wasomi wenye mahusiano na mabwanyenye hao na wazalendo wengine. Kwa kuongozwa na Chama cha Kikomunisti cha China, vyama mbalimbali vya kidemokrasia vimefanya juhudi kubwa katika kuanzisha China Mpya, kujenga China Mpya, uzoefu mkubwa wa kufanya utafiti kuhusu njia ya kufanya mageuzi na kutimiza Ndoto ya China, ambapo vinachangia zaidi mambo makubwa ya kujipatia uhuru wa kitaifa, ukombozi wa watu na ustawi wa nchi, na maisha ya furaha ya wananchi.