China yatoa wito kwa nchi wanachama wa kundi la G20 kuendeleza ushirikiano
2021-06-30 08:53:52| CRI

Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi amezitaka nchi wanachama wa kundi la G20 kukuza moyo wa ushirikiano na kutoa mapendekezo ya kufanya juhudi kwa pamoja.

Bw. Wang Yi alisema hayo jana aliposhiriki kwenye mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje wa nchi wanachama wa kundi la G20 uliofanyika kwa njia ya video, Amesema, hivi sasa hali ya janga la COVID-19 duniani bado ni tete, na viwango vya ufufukaji wa uchumi vinatofautiana katika sehemu mablimbali za dunia, nchi wanachama wa G20 zinapaswa kushikilia kufanya ushirikiano na kutekeleza uongozi katika mapambano dhidi ya janga hilo, kutekeleza mafanikio ya mkutano wa Shirika la afya duniani WHO, kuimarisha ushirikiano katika sekta ya chanjo, matibabu, kinga na udhibiti wa pamoja, na kutoa msaada zaidi kwa nchi zinazoendelea.