Rais Xi Jinping anasema Wachina hawatakubali uonevu wa kigeni, ukandamizaji au utwezaji
2021-07-01 09:39:44| cri

Rais Xi Jinping wa China ambaye pia ni katibu mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), amesema kamwe wachina hawataruhusu nguvu yoyote ya kigeni kuwaonea, kuwakandamiza au kuwatweza.

Akiongea kwenye maadhimisho ya miaka 100 ya Chama cha Kikomunisti cha China, Rais Xi amesema mtu yeyote atakayejaribu kufanya hivyo atakumbana na ukuta mkubwa wa chuma uliojengwa na watu zaidi ya bilioni 1.4 wa China.

Rais Xi amesema China haijawahi kuonea, kudhulumu, au kuwatisha watu wa nchi nyingine yoyote, na kamwe haitafanya hivyo. Amesema siku zote China imekuwa ikifanya kazi ya kulinda amani ya ulimwengu, kuchangia maendeleo ya dunia, na kulinda utulivu wa kimataifa, na ametoa mwito wa kuhimiza ujenzi wa jumuiya ya binadamu yenye mustakbali wa pamoja.