Xi Jinping: Maendeleo mapya ya China yatoa fursa mpya kwa dunia
2021-07-01 12:12:52| cri

 

Rais Xi Jinping wa China leo amesema, maendeleo mapya ya China yatatoa fursa mpya kwa dunia.

Akihutubia katika maadhimisho ya miaka 100 tangu kuanzishwa kwa Chama cha Kikomunisti cha China mapema leo rais Xi amesema China lazima ishikilie njia ya kujiendeleza kwa amani, kukuza ujenzi wa uhusiano wa aina mpya wa kimataifa, ujenzi wa jumuiya ya binadamu yenye hatma ya pamoja, na kusukuma mbele maendeleo yenye kiwango cha juu ya “Ukanda Mmoja, Njia Moja”.

Pia amesisitiza kuwa, China siku zote ni mjenzi wa amani ya dunia, mchangiaji wa maendeleo ya dunia, na mlinzi wa utaratibu wa dunia, na Chama cha Kikomunisti cha China kitashikilia kufanya ushirikiano wa kunufaishana na kupinga umwamba.