China yaitaka Japan iwe makini katika kushughulikia majitaka ya nyuklia
2021-07-01 09:10:28| CRI

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Wang Wenbin amesema China inaionya Japan kwa mara nyingine tena kuwa ushughulikiaji wa majitaka ya kinyuklia, unahusiana afya ya watu wa Japan na wa dunia nzima, unahusiana na usalama wa mazingira ya kiikolojia ya baharini, na ni lazima ufanyike kwa umakini mkubwa.

Juni 29, Bunge la Korea Kusini lilipitisha azimio la kuilaani vikali serikali ya Japan kutokana na uamuzi wake wa kumwaga baharini majitaka ya kinyuklia yaliyochafuliwa katika kituo cha umeme wa nyuklia cha Fukushima, na kuitaka Japan ifute uamuzi huo mara moja.

Bw. Wang Wenbin amesema, China inaunga mkono msimamo wa haki wa Korea Kusini, na kuitaka Japan ifute uamuzi wa makosa, na kurudi mapema iwezekanavyo kwenye njia sahihi ya kufanya majadiliano kamili na wadau mbalimbali wa jumuiya ya kimataifa na Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki IAEA.