Xi Jinping: Uongozi imara wa CPC unatakiwa kulindwa
2021-07-01 09:32:00| cri

Xi Jinping: Uongozi imara wa CPC unatakiwa kulindwa_fororder_1127614524_16251035067921n

Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China CPC Xi Jinping amesema uongozi imara wa CPC unatakiwa kulindwa.

Kwenye hafla ya kuadhimisha miaka 100 ya CPC iliyofanyika leo hapa Beijing, Bw. Xi Jinping ambaye pia ni rais wa China na mwenyekiti wa Kamati Kuu ya kijeshi ya CPC, amesema uongozi wa Chama hicho ni sifa ya kimsingi ya ujamaa wenye umaalum wa China na kutoa nguvu kubwa kwa mfumo huo. Ameongeza kuwa uongozi wa CPC ni msingi na damu ya Chama na nchi, na una uhusiano wa karibu na maslahi na mustakbali wa watu wote wa China.

Xi Jinping: Uongozi imara wa CPC unatakiwa kulindwa_fororder_1127614286_1625101237040_title0h