Xi Jinping: Jaribio lolote la kutenganisha Chama cha Kikomunisti cha China na watu wa China halitafanikiwa kamwe
2021-07-01 12:09:31| cri

 

Rais Xi Jinping wa China amesema katika Mkutano wa Maadhimisho ya Miaka 100 tangu kuanzishwa kwa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) kuwa, daima Chama hicho kinawakilisha maslahi ya kimsingi ya wananchi, na kuishi kwa kutegemeana na wananchi, na hakina maslahi yoyote maalum, na kamwe hakiwakilishi maslahi ya kundi lolote lenye mamlaka, na watu wenye hadhi maalum. Ameongeza kuwa, jaribio lolote la kutenganisha chama hicho na watu wa China kwamwe halitafanikiwa .

Pia amesisitiza kuwa, CPC lazima kizingatie madhumuni ya kimsingi ya kuwahudumia wananchi kwa moyo wote, kufuata msimamo wa wananchi, na kuhimiza mchakato wa maendeleo ya pande zote ya binadamu, pia kuhakikisha wananchi wote wanapata maendeleo makubwa zaidi na kutajirika kwa pamoja.