Ofisa mwandamizi wa WHO aipongeza China kwa kupata cheti cha kutokomeza ugonjwa wa malaria
2021-07-01 09:23:15| CRI

Mkurugenzi mkuu msaidizi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) anayeshughulikia Huduma za Afya kwa Wote na Magonjwa ya Kuambukiza na Yasiyo ya Kuambukiza Dkt. Ren Minghui, ameipongeza China kwa kupata cheti cha kutokomeza ugonjwa wa malaria kutoka kwa WHO, akisema hatua hiyo inatia moyo kwa kutimiza lengo la kutokuwa na ugonjwa wa malaria duniani. 

Dkt. Ren amesema mafanikio haya yaliyopatikana kwa juhudi kubwa, ni matokeo ya juhudi za mwanasayansi wa China Profesa Tu Youyou, na wataalamu wa afya ya umma na wafanyakazi wa afya wa China.

WHO jana lilitoa rasmi cheti cha kutokuwa na malaria kwa China kutokana na kufanikiwa kutokomeza ugonjwa huo baada ya juhudi za miaka 70.