Xi Jinping: China yakamilisha ujenzi wa jamii yenye maisha bora kwa pande zote
2021-07-01 09:32:54| cri

Katibu mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China CPC Xi Jinping ametangaza kuwa China imetimiza lengo la kwanza la karne, yaani kujenga jamii yenye maisha bora kwa pande zote.

Kwenye hafla ya kuadhimisha miaka 100 ya CPC iliyofanyika leo hapa Beijing, Xi Jinping ambaye pia ni rais wa China na mwenyekiti wa Kamati Kuu ya kijeshi ya CPC, amesema hii inamaanisha kuwa China imetatua tatizo la umaskini uliokithiri nchini China na inaelekea kutimiza lengo la pili la karne la kuijenga China kuwa nchi ya kisasa ya kijamaa yenye nguvu katika pande zote.