Mkuu wa Baraza la usalama la UM amesema kama hali ya afya itaruhusu mikutano yote itakuwa ya ana kwa ana
2021-07-02 08:53:11| CRI

Balozi wa Ufaransa na mkuu wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa Bw. Nicolas de Riviere, amesema mikutano ya baraza la usalama la Umoja wa mataifa itafanyika ana kwa ana kama hali ya afya itaruhusu.

Bw. de Riviere amesema mwezi huu wa Julai kama hali itaruhusu hakutakuwa na mikutano inayofanyika kwa njia ya video, kwa hiyo washiriki watatakiwa kuwepo mikutanoni wenyewe ana kwa ana, hata mawaziri wataalikwa.

Amesema mikutano ya ana kwa ana ni muhimu kwa kuwa baraza la usalama linajumuisha wajumbe 15, ambao lengo lake ni kutafuta muafaka kutatua migogoro. Balozi huyo amesema anatumai kuwa mabalozi hawatakuwa wanatoa hotuba baada ya hotuba, jambo ambalo halisaidii sana.

Balozi huyo amesema kuna mikutano miwili inayofuata mmoja unafanyika Julai 6 na mwingine Julai 16.