Hotuba ya Rais Xi kwenye maadhimisho ya miaka 100 ya CPC imekuwa na mwitikio mzuri duniani
2021-07-02 08:36:57| CRI

Jumuiya ya kimataifa imeonyesha mwitikio mzuri wa hotuba aliyotoa Rais Xi Jinping wa China kwenye sherehe za maadhimisho ya miaka 100 ya Chama cha Kikomunisti cha China CPC zilizofanyika jana mjini Beijing, ambayo imekumbusha historia ya maendeleo ya CPC na kutupia macho mustakbali mzuri wa China kutimiza ustawishwaji mpya wa taifa.

Viongozi, maofisa na wataalamu wa nchi za nje wameona kuwa katika miaka 100 iliyopita, CPC kimewaongoza watu wa China kupitia changamoto mbalimbali na kupata mafanikio makubwa, kikiandika ukurasa uliotukuta katika historia ya taifa la China na ya ustaarabu wa binadamu.

Bw. Cavince Adhere, mtaalamu wa mahusiano ya kimataifa wa Kenya, amesifu falsafa ya CPC ya kutoa kipaumbele kwa maslahi ya umma na mchango wa CPC kwenye maendeleo ya binadamu na ya dunia nzima, akisema chini ya uongozi wa CPC, China imekuwa mtetezi thabiti wa mfumo wa pande nyingi.

Naye mkurugenzi wa Kituo cha Utafiti wa China katika Chuo kikuu cha Dar es Salaam nchini Tanzania profesa Humphrey Moshi, amesema uongozi wa CPC siku zote umekuwa na ruwaza ya kuona mbali na kuzingatia maslahi ya umma, ndiyo maana kumekuwa na mawasiliano ya karibu kati ya CPC na watu wa China, ambayo yamewezesha utekelezaji wa haraka wa maamuzi nchini kote.