Wanaanga wa China wakamilisha jukumu la kwanza katika ujenzi wa kituo cha anga ya juu cha China
2021-07-05 08:58:17| CRI

Wanaanga wa China wamemaliza jukumu la kwanza la ujenzi wa nje wa kituo cha anga ya juu cha China na kurejea kwenye chombo cha anga ya juu cha Tianhe.

Taarifa iliyotolewa jana na Mamlaka ya Anga za Juu ya China (CMSA) imesema, jukumu hilo limekamilika kwa mafanikio, na kuongeza kuwa, wanaanga hao walitumia saa 7 kukamilisha majukumu yote yaliyopangwa.

Mamlaka hiyo imesema, hatua hiyo imeweka msingi muhimu kwa shughuli nyingine za nje kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha anga ya juu cha China.