Watu 10 wauawa mjini Chicago kwenye matukio ya matumizi ya bunduki wikiendi iliyopita
2021-07-05 15:02:46| Cri

Kutokana na taarifa ya habari za vyombo vya habari mbalimbali vya Marekani, matukio mengi ya vurugu za matumizi ya bunduki yametokea mjini Chicago, Marekani kuanzia usiku wa tarehe 2 mwezi huu. Katika wikiendi moja tu iliyopita, vurugu hizo zimesababisha watu wasiopungua 38 kupigwa risasi na 10 kati yao wameuawa. Usiku wa tarehe 3, mvulana mmoja mwenye umri wa 19 alipigwa risasi tano na mwanaume mwingine alipigwa risasi alipokuwa anatembea barabarani na wote wamekufa, na mwingine aliuawa na wawili kujeruhiwa katika eneo moja karibu na mji wa Chicago. Ofisa mkuu wa Polisi wa Chicago amesema wikiendi iliyopita imekuwa ni wikiendi yenye taabu zaidi kwa polisi kwa mwaka huu.