Rais Xi Jinping wa China kuhudhuria Mkutano wa viongozi wa Chama cha CPC na vyama mbalimbali duniani
2021-07-05 10:07:32| Cri

Msemaji wa Idara ya mawasiliano na nje ya Kamati kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China CPC Hu Zhaoming ametangaza kuwa, Mkutano wa Viongozi wa Chama cha CPC na Vyama mbalimbali duniani utafanyika kesho tarehe 6 kwa njia ya video, ambapo rais Xi Jinping wa China atahudhuria na kutoa hotuba mjini Beijing. Kauli mbiu ya mkutano huo ni “Kuwatafutia wananchi neema: Ni Wajibu wa Vyama”, na viongozi zaidi ya 500 wa vyama na mashirika ya kisiasa kutoka nchi zaidi ya 160 duniani pamoja na wanachama zaidi ya elfu moja wa vyama watahudhuria mkutano.

  Mkutano huo ni shughuli muhimu ya kidiplomasia ya pande nyingi katika wakati wa maadhimisho ya miaka 100 tangu kuanzishwa kwa Chama cha Kikomunisti cha China, ambao unalenga kuimarisha mawasiliano ya uzoefu wa utawala wa nchi kati ya vyama mbalimbali vya kisiasa duniani, ili kukabiliana na changamoto zinazotokana na mabadiliko makubwa ya hali ya dunia na janga la COVID-19, kuongeza uwezo wa kuwatafutia wananchi furaha, kuhimiza amani na maendeleo ya dunia, na kuhimiza ujenzi wa Jumuiya ya Binadamu yenye Hatma ya Pamoja.