Rais wa Baraza la Uchumi na Jamii la UN asema kinachotetewa na China ni ukweli wa hali yenye pande nyingi
2021-07-05 09:12:20| cri

Rais wa Baraza la Uchumi na Jamii la Umoja wa Mataifa Bw. Munir Akram amesema, China ni mlinzi wa kweli wa hali yenye pande nyingi, na inachotetea ni ukweli wa hali yenye pande nyingi. Amesema njia hii inavutia nchi nyingi duniani.

Kwa maoni ya Akram, wito wa China wa kutekeleza hali yenye pande nyingi ni kutafuta suluhisho la masuala ya kimataifa kupitia mchakato wenye haki na shirikishi. Hali hiyo inayotetewa na China ni wazo lililovutia pande nyingi zinazohitaji uongozi wa Umoja wa mataifa na uhusiano wa pande nyingi.