Balozi wa Tanzania: Mkoa wa Xinjiang, China umepata maendeleo makubwa
2021-07-05 12:16:09| Cri

Kutoa kipaumbele kwa maslahi ya umma ndio msingi wa CPC kukubalika na kupendwa na wananchi_fororder_坦桑尼亚驻华大使

Kwa kweli huwezi kuita mkoa wa Xinjiang mkoa maskini, pato la mkoa wa Xinjiang linazidi pato la nchi yoyote ya Afrika, hakuna nchi inayoifikia, hata nchi zenye uchumi mkubwa wa Afrika, za Afrika Kusini na Nigeria pato lao halifikii GDP ya mkoa wa Xinjiang, kwa hiyo sio mkoa maskini.

Hayo yamesemwa na Balozi wa Tanzania nchini China Bw. Mbelwa Kairuki. Amesema, “mkoa wa Xinjiang ni mkoa wenye watu wa makabila tofauti, kuna makabila madogo madogo, ambao kuna watu wanawatumia kufanya siasa kusema watu hawa wanabaguliwa, wanazuiwa kutumia lugha zao, au wananyanyaswa. Lakini tulichojifunza ni kuwa kuna watu wanaojaribu kufanya jitihada kuwashawishi watu hawa wajitenge, kitu ambacho China ikiwa ni nchi huru haiwezi kukubali, na nchi yoyote ile haiwezi kukubali kuwa kuna sehemu ya mkoa wenu unataka kujitenga unataka kuwa nchi, haiwezekani.

Kwa hiyo China imekuwa na msimamo thabiti kama watu hao ni sehemu ya China, na watapewa haki na stahili zote kama raia wa China. Ni kweli idadi kubwa ya watu wanaoishi kule ni Waislamu, na kumekuwa na upotoshaji kuwa Wasialamu wananyimwa haki zao za kusali na kuabudu…Lakini tumeona kuna misikiti kadhaa na wananchi wanaruhusiwa kwenye kusali wakati wowote, na tumekutana na Maimam wa misikiti ile, wametuthibitishia kuwa wako huru kuabudu, kwa hiyo hizi taarifa zinazotolewa kwenye vyombo vya magharibi zinakuwa na ajenda yake.

Lakini kitu kimoja ambacho ni dhahiri, kwamba kuna baadhi ya watu walikuwa wanadhamini vikundi vichache wafanye matukio ya kigaidi, kuua watu kuumiza watu, serikali ya China imechukua hatua, imechukua hatua kama ambavyo serikali nyingine yoyote itachukua hatua, kama kuna watu wanavunja sheria wanafanya ugaidi, hatua za kisheria zinachukuliwa. Hizo hatua ndio baadhi wanataka kupigia kelele kuwa hawa wanavunja haki za binadamu.

Lakini watu haohao hatukuwasikia wakipiga kelele, wakati taifa moja lililopata tatizo la ugaidi lilivyoendesha operesheni kubwa tu, tena dunia nzima wanaenda kwenye nchi nyingine wanachukua watu wanawapeka kwenye nchi nyingine, kwa kigezo kuwa wanapambana na ugaidi, sasa China ikichukua hatua ndani ya nchi yake kupambana na ugaidi, kwa kweli itakuwa si sahihi kuwalaumu, kwa sababu mpaka ukienda ukaona kwenye jumba la makumbusho pale Xinjiang, matukio ya kigaidi yaliyofanyika na idadi ya watu walioathiriwa, sasa tunapoongea haki za binadamu basi pia tuongee haki za binadamu za wahanga wa matukio ya ugaidi na wao, hao nani anawasemea?”