Watu 17 wafariki katika ajali ya ndege ya kijeshi nchini Ufilipino
2021-07-05 08:56:55| CRI

Waziri wa ulinzi wa Ufilipino Delfin Lorenzana jana amesema, watu 17 wamefariki na wengine 40 kujeruhiwa katika ajali ya ndege ya kijeshi iliyotokea jana kusini mwa Ufilipino.

Bw. Lorenzana amesema, ripoti ya awali ya ajali hiyo inaonyesha kuwa, wakati wa ajali hiyo, ndege hiyo ilikuwa imebeba watu 92, wakiwemo marubani 3 na wafanyakazi 5. Mpaka sasa miili 17 imepatikana na kazi ya uokoaji inaendelea.