China yakanusha kauli ya Marekani na Uingereza inayodai kuwa China inajaribu kudhibiti mashirika ya kimataifa
2021-07-06 08:32:23| cri

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya nje ya China Bw. Wang Wenbin amesema, taarifa zilizotolewa na baadhi ya viongozi wa Marekani na Uingereza kuwa China inajaribu kudhibiti mashirika ya kimataifa hazina ukweli wowote.

Wang Wenbin amesema, China inashikilia kulinda na kutekeleza kihalisi uhusiano wa pande nyingi, na kuongeza kuwa, China inajitahidi kushiriki kwenye kazi za mashirikia ya kimataifa.

Ametolea mfano katika sekretarieti ya Umoja wa Mataifa, akisema hivi sasa kuna raia 548 wa China wanaofanya kazi katika sekretarieti hiyo, ikiwa ni asilimia 1.5 ya wafanyakazi wote, ambayo ni sawa na asilimia 22 ya idadi ya wafanyakazi wa Marekani na asilimia 70 ya wafanyakazi wa Uingereza.Amesema China itashirikiana na nchi zinazoendelea, kuendelea kushiriki kwenye kazi za mashirika ya kimataifa, na kutoa mchango kwa ajili ya kuhimiza ushirikiano wa kimataifa na kutekeleza kihalisi uhusiano wa pande nyingi.