Rais wa China asisitiza kupinga hatua za upande mmoja na kukataa umwamba duniani
2021-07-06 22:12:45| cri

Rais Xi Jinping wa China ambaye pia ni katibu mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), leo ametoa wito wa kuwepo kwa juhudi za pamoja za kupinga vitendo vya kujichukulia hatua kwa upande mmoja, kwa kivuli cha hatua za pamoja, na kusema tunatakiwa kukataa umwamba na siasa za kutaka nguvu.

Rais Xi amesema hayo mjini Beijing wakati akitoa hotuba kwenye Mkutano wa Chama cha Kikomunisti cha China CPC na Vyama vingine vya Siasa duniani, mkutano uliofanyika kwa njia ya video.

Rais Xi pia amesema CPC iko tayari kutoa majawabu ya China kwa kufuata mtazamo na vitendo katika mchakato wa kupunguza umaskini duniani.

Ameongeza pia kuwa China itajitolea kusaidia ushirikiano wa kimataifa kwenye mapambano dhidi ya COVID-19, na kusema China pia itafanya juhudi zaidi ili kuhakikisha kuwa inatimiza ahadi yake ya kuondoa gesi ya kaboni.