Rais wa China ahutubia mkutano wa kilele wa viongozi wa CPC na vyama vya siasa duniani
2021-07-07 08:53:26| CRI

 

 

Mkutano wa kilele wa viongozi wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na vyama vya siasa vya nchi mbalimbali duniani umefanyika kwa njia ya video, na kuhudhuriwa na viongozi na wawakilishi zaidi ya elfu 10 wa vyama zaidi ya 500 vya kisiasa kutoka nchi zaidi ya 160 duniani.

Akihutubia mkutano huo, Rais Xi Jinping wa China ambaye pia ni katibu mkuu wa CPC amesisitiza kuwa maendeleo siyo haki ya nchi chache duniani, bali ni haki ya nchi zote na vyama vya siasa vinapaswa kuzihimiza nchi mbalimbali duniani kukuza ushirikiano wa maendeleo, kuwawezesha wananchi wao kunufaika na maendeleo, kuongeza usawa, ufanisi na uratibu wa maendeleo ya dunia, na kupinga kwa pamoja mtu yeyote kuweka vizuizi vya teknolojia, kuleta pengo la maendeleo ya sayansi na teknolojia, na kutenganisha juhudi za maendeleo. Pia amesema, CPC kitahimiza kukamilisha usimamizi wa mambo ya kimataifa kwa hatua madhubuti, na kutoa mchango mpya kwa juhudi za binadamu kukabiliana na changamoto kwa pamoja.

Pia Rais Xi amesema, kuondoa umaskini ni lengo muhimu la vyama vya siasa vya nchi mbalimbali. China imetimiza lengo la kutokomeza umaskini uliokithiri, na inapenda kutoa uzoefu wake kwa mchakato wa kuondoa umaskini duniani.