Rais wa Haiti auawa kwa kupigwa risasi katika makazi yake
2021-07-08 08:36:46| CRI

Waziri Mkuu wa Mpito wa Haiti amesema, Rais wa nchi hiyo, Jovenel Moise ameuawa kwa kupigwa risasi akiwa nyumbani kwake mapema jana.

Hayati Moise ameiongoza Haiti, nchi masikini zaidi katika bara la Amerika, kwa amri ya mahakama baada ya uchaguzi wa wabunge uliopangwa kufanyika mwaka 2018 kuahirishwa.