Rais Xi Jinping atoa mwito wa kufanyika juhudi zaidi kuleta mtindo mpya wa maendeleo
2021-07-09 21:53:11| cri

Rais Xi Jinping amesisitiza kuwepo kwa juhudi za kuhimiza mtindo mpya wa maendeleo, kuhimiza kuipa uhai sekta ya mbegu na kuendeleza ulinzi wa kiikolojia na mazingira, pamoja na maendeleo endelevu ya uwanda wa juu wa Qinghai-Tibet.

Rais Xi, ambaye pia ni katibu mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China na mwenyekiti wa Kamati ya Kijeshi, amesema hayo leo wakati akiendesha mkutano wa 20 wa kamati kuu kuhusu kuimarisha mageuzi ya jumla.