Viongozi wa China na Sudan Kusini watumiana salamu za pongezi kwa kutimiza miaka 10 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kibalozi
2021-07-09 12:09:51| Cri

Rais Xi Jinping wa China leo ametumiana salamu za pongezi na rais Salva Kiir wa Sudan Kusini, ili kusherehekea miaka kumi tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kibalozi kati ya nchi hizo mbili.

Katika salamu zake Rais Xi ameeleza kuwa, China inaweka mkazo mkubwa katika kukuza uhusiano kati ya China na Sudan Kusini, na kupenda kushirikiana na rais Kiir kuimarisha uaminifu wa kisiasa kati ya pande mbili, kuwasiliana na kushirikiana pamoja katika sekta mbalimbali chini ya mfumo wa “Ukanda Mmoja, Njia Moja”, ili kunufaisha nchi hizo mbili na wananchi wao.

Mwenzake Rais Kiir ameeleza kuwa Sudan Kusini inatarajia kuzidi kuimarisha uhusiano wenye kiwango cha juu kati ya pande mbili.

Siku hiyo waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi na waziri wa Ushirikiano wa Kimataifa wa Sudan Kusini Bibi Beatrice Wani-Noah pia walitumiana salamu za pongezi kwa ajili ya maadhimisho hayo.

Bw. Wang Yi amesema anapenda kushirikiana na Bibi Beatrice kuhimiza uhusiano wa kirafiki na ushirikiano kati ya pande mbili hadi kufikia kiwango kipya.

Naye Bi. Beatrice anaamini uhusiano kati ya pande hizo mbili utazidi kuimarishwa na kuwanufaisha watu wa nchi hizo mbili.