Waziri wa mambo ya nje wa China kutembelea nchi tatu za Asia ya Kati
2021-07-09 21:54:49| cri

Katibu wa baraza la kitaifa Mjumbe wa taifa wa China ambaye pia ni waziri wa mambo ya nje Bw. Wang Yi atatembelea Turkmenistan, Tajikistan na Uzbekistan kuanzia Julai 12 hadi 16 mwezi huu.

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Wang Wenbin amesema Ijumaa kuwa, wakati wa ziara hiyo, Bw.Wang Yi atahudhuria mkutano wa Baraza la Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Shirika la Ushirikiano la Shanghai (SCO), Mkutano wa Kikundi cha Mawasiliano cha SCO-Afghanistan, pamoja na mkutano wa kimataifa wa uunganisho uitwao “Asia ya Kati na Kusini: uunganishaji wa kikanda, changamoto na fursa”.

Hali ya usalama nchini Afghanistan iliyokumbwa na vita imekuwa mbaya wakati wanamgambo wa Taliban wakiendelea na mapigano makali dhidi ya vikosi vya serikali. Wiki hii zaidi ya wanajeshi 1,000 wa Afghanistan walikimbilia Tajikistan kukwepa mashambulizi ya Taliban katika eneo la Kaskazini mwa Afghanistan.