Rais wa China atoa salamu za rambirambi kwa mwenzake wa Russia kutokana na ajali ya ndege ya abiria
2021-07-09 12:18:48| Cri

Rais Xi Jinping wa China ametoa salamu za rambirambi kupitia simu kwa mwenzake wa Russia Vladimir Putin kutokana na ajali ya kuanguka kwa ndege ya abiria nchini Russia.

Rais Xi amesema anahuzunishwa na ajali hiyo ambayo ilisababisha vifo vya abiria na wafanyakazi wote wa ndege hiyo. Kwa niaba ya serikali ya China na watu wake rais Xi ametoa salamu za rambirambi kwa msiba huo, na kuwapa pole ndugu na jamaa wa waliofariki.