Shirika la IAEA na Japan zasaini makubaliano kuhusu kukagua usalama wa mpango wa kutoa maji machafu ya nyuklia
2021-07-09 12:20:00| Cri

Shirika la Nishati ya Atomiki la Kimataifa (IAEA) jana lilisaini makubaliano na Japan ya kuisaidia kitekenolojia katika mchakato wa ukaguzi na usimamizi wa kutoa maji machafu ya nyuklia.

Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo Bw. Bw. Rafael Mariano Grossi alisema kuwa shirika la IAEA litaupa umuhimu mkubwa usimamizi na ukaguzi wa utekelezaji wa mpango ya Japan. Wataalam wa IAEA watakagua kama utoaji wa maji machafu ya nyuklia unatekelezwa kwa njia ya usalama au la. Ni muhimu kuwahakikishia watu nchini Japan na sehemu nyingine za dunia, haswa katika nchi jirani kwamba maji taka ya nyuklia hayataleta tishio kwao.

Japani ilipanga kuanza kutoa maji taka ya nyuklia ndani ya miaka miwili, na mchakato wote unaendelea kwa miaka miongo kadhaa. Kulingana na makubaliano hayo, kikundi cha wataalam cha IAEA kinatarajiwa kusafiri kwenda Japan kwa mara ya kwanza ndani ya mwaka huu.