Hafla ya kuadhimisha miaka 20 ya kusainiwa kwa mkataba wa ushirikiano wa kirafiki kati ya China na Russia yafanyika
2021-07-12 08:36:49| Cri

Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi amehudhuria hafla ya kuadhimisha miaka 20 tangu kusainiwa kwa Mkataba wa Ujirani Mwema na Ushirikiano wa Kirafiki kati ya China na Russia.

Kwenye hotuba yake, Wang amesema katika miongo miwili iliyopita, chini ya muongozo wa mkataba huo, uhusiano kati ya China na Russia umeendelea kuwa imara dhidi ya changamoto na hatari, na kufikia kwenye kiwango cha juu kabisa kihistoria. Amesema nchi hizo mbili zinapaswa kuaminiana zaidi kisiasa, kufanya ushirikiano halisi, kuongeza mawasiliano kati ya watu na watu na ya kiutamaduni, na kuimarisha uratibu wa kimkakati ili kufungua ukurasa mpya kwenye uhusiano wa pande mbili katika mwanzo mpya wa kihistoria.

Mwezi uliopita Balozi wa Russia nchini China Andrey Denisov alisema, viongozi wa nchi hizo mbili walitoa taarifa ya pamoja wakiamua kuongeza muda wa mkataba huo, na kuweka malengo makubwa zaidi ya kutafuta maendeleo katika ushirikiano kati ya nchi hizo. Amesema Russia itashirikiana na China kufanya kila iwezalo ili kutimiza malengo hayo.