Viongozi wa China na Korea Kaskazini wapongezana kwa maadhimisho ya Miaka 60 ya Makubaliano ya Urafiki na Ushirikiano
2021-07-12 09:05:36| Cri

Rais Xi Jinping wa China na Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un walitumiana salamu za pongezi Jumapili katika Maadhimisho ya Miaka 60 tangu kusainiwa kwa Makubaliano ya Urafiki, Ushirikiano na Misaada kati ya pande mbili.

Katika salamu zake, rais Xi amesisitiza kuwa kasi ya mabadiliko makubwa duniani ambayo hayajawahi kuonekana katika kipindi cha miaka 100 iliyopita inazidi kuongezeka, na China iko tayari kushirikiana na Korea Kaskazini, kuimarisha mawasiliano ya kimkakati, kupanga malengo ya maendeleo ya uhusiano kati ya pande mbili na kuinua kiwango cha Ushirikiano wa kirafiki kati ya nchi mbili, ili kunufaisha zaidi nchi hizo mbili na watu wao.

Naye mwenzake Kim amesema kusainiwa kwa makubaliano hayo kunaonesha imani thabiti ya serikali na watu wa pande mbili ya kuhimiza maendeleo ya muda mrefu ya urafiki kati ya nchi hizo.