Kampuni za China kupeleka chanjo milioni 110 za COVID-19 kwenye Mpango wa COVAX
2021-07-13 09:16:15| CRI

Muungano wa Chanjo Duniani (Gavi) jana ulitangaza kuwa kampuni mbili za utengenezaji dawa za China zitatoa chanjo milioni 110 za COVID-19 kwa washiriki wa mpango wa COVAX ili kukabiliana na changamoto zinazotokana na virusi vipya vya Delta.

Chanjo zinazotengenezwa na kampuni za Sinopharm na Sinovac za China zimeidhinishwa na Shirika la Afya Duniani (WHO) mapema mwaka huu kwa ajili ya matumizi ya dharura.

Gavi imetangaza kwamba imesaini makubaliano na kampuni hizo mbili za China kwa ajili ya kununua chanjo zao, ambapo kulingana na makubaliano hayo dozi milioni 60 za chanjo za Sinopharm zitapatikana kuanzia Julai hadi Oktoba, na dozi nyingine milioni 50 za chanjo za Sinovac zitapatikana kuanzia Julai hadi Septemba mwaka huu.