China ni nchi iliyotoa chanjo nyingi zaidi za COVID-19 duniani
2021-07-13 09:18:12| CRI

China imetoa dozi milioni 500 za chanjo ya COVID-19 na malighafi kwa nchi na sehemu zaidi ya 100 duniani, kiasi ambacho ni sawa na moja ya sita ya chanjo hizo zilizozalishwa kote duniani.

Akifahamisha kuhusu China kutoa chanjo hiyo kwa nchi za nje, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Bw. Zhao Lijian jana hapa Beijing alisema China inatekeleza ahadi muhimu iliyotolewa na rais Xi Jinping wa China ya kufanya chanjo kuwa bidhaa ya umma duniani, kushikilia wazo la kujenga jumuiya ya binadamu yenye hatma ya pamoja na kutoa chanjo kwa nchi za nje katika msingi wa uwazi na jumuishi.

Bw. Zhao ameongeza kuwa China ni nchi iliyotoa chanjo nyingi zaidi za COVID-19 kwa nchi zinazoendelea na wenzi wa ushirikiano wa chanjo wapo kote duniani.