China yashangazwa na madai ya Marekani kuwa inaongoza duniani katika mapambano dhidi ya COVID-19
2021-07-14 13:57:06| cri

 

 

Msemaji wa wizara ya mambo ya China Zhao Lijian ameeleza kushangazwa na ripoti iliyotolewa na Shirika la habari la Marekani Bloomberg kuhusu ufanisi wa kazi za kukabiliana na janga la COVID-19 za nchi mbalimbali duniani, na kusema ripoti hiyo haifuati ukweli halisi.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, Marekani inashika nafasi ya kwanza duniani kwa ufanisi wake katika kukabiliana na janga la COVID-19, huku China ikishika nafasi ya nane.

Zhao amesema, ili kuiwezesha Marekani kupata nafasi ya kwanza, ripoti hiyo imepuuza idadi ya wagonjwa na vifo vilivyotokana na janga hilo, na kuchukulia vizuizi na hatua za kuzuia virusi mipakani kama sababu ya kupunguza alama, kitendo ambacho hakijafuata hali halisi, wala hakiheshimu sayansi na maisha ya watu.