Rais Xi asema China iko tayari kuzisaidia Ukraine na Uturuki kupambana na janga la COVID-19
2021-07-14 10:12:32| CRI

Rais Xi Jinping wa China amesema China iko tayari kuimarisha zaidi ushirikiano na Ukraine kwenye masuala ya chanjo na dawa za jadi za China, ili kuisaidia nchi hiyo kushinda janga la COVID-19.

Akiongea kwa njia ya simu na mwenzake wa Ukrane Volodymyr Zelensky, rais Xi amebainisha kuwa tangu China na Ukraine zianzishe ushirikiano wa kimkakati miaka 10 iliyopita, uhusiano wa pande mbili umedumisha kasi nzuri na imara katika maendeleo, na ushirikiano kwenye nyanja mbalimbali umezaa matunda, na kuwanufaisha watu wa nchi mbili.

Wakati huohuo rais Xi ameongea na mwenzake wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan na kusema China iko tayari kushirikiana kwa kina na Uturuki kwenye suala la chanjo ili kuisaidia nchi hiyo iondokane na janga la COVID-19 mapema. Amesema ushirikiano wa karibu kati ya pande mbili kwenye mapambano dhidi ya COVID-19 umepiga hatua mpya, na kusisitiza kuwa pande zote mbili zinapaswa kupinga kufanya suala la chanzo cha virusi kuwa la kisiasa.