Dozi bilioni 11 za chanjo zahitajika kuchanja asilimia 70 ya watu duniani ili kumaliza COVID-19
2021-07-14 10:08:18| CRI

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres amesema dozi bilioni 11 za chanjo zinahitajika kwa ajili ya kuchanja asilimia 70 ya watu duniani ili kumaliza janga la COVID-19.

Bw. Guterres amesema hayo kwenye ufunguzi wa mkutano wa mawaziri wa Jukwaa la Ngazi ya Juu la Kisiasa kuhusu Maendeleo Endelevu, ambalo ni jukwaa kuu la kutathmini utekelezaji wa Ajenda ya 2030 ya Maendeleo Endelevu na Malengo yake 17 ya Maendeleo Endelevu.

Ameongeza kuwa kila mahali, na kila mtu lazima apate chanjo za COVID-19, kufanyiwa vipimo, kutibiwa na kusaidiwa. Na kwamba Muungano wa Chanjo Duniani (Gavi) na kituo chake cha COVAX, unatoa matumaini kwenye maendeleo na utoaji wa chanjo, kupitia utaratibu wa usawa duniani.