Nchi zinazoendelea duniani zalaani ubaguzi wa rangi dhidi ya watu wenye asili ya Afrika na Asia
2021-07-14 08:38:22| Cri

Katika Mkutano wa 47 wa Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa kuhusu kulinda haki za binadamu za waafrika na watu wenye asili ya Afrika, nchi zinazoendelea zimelaani ubaguzi wa kimfumo na ubaguzi wa rangi, zikiitaka jamii ya kimataifa kuongeza nguvu katika kupambana na ubaguzi na matumizi ya nguvu dhidi ya watu wenye asili ya Afrika na Asia.

Mwakilishi wa kudumu wa China katika Ofisi ya Umoja wa Mataifa huko Geneva Balozi Chen Xu akiwakilisha nchi 50 duniani ametoa hotuba katika mkutano huo akieleza kuwa, waafrika na waasia pamoja na watu wenye asili ya Afrika na Asia wanakabiliwa na ubaguzi wa kimfumo, ubaguzi wa rangi na uhalifu wa chuki katika muda mrefu uliopita. Ameyasisitiza mashirika mbalimbali ya haki za binadamu kuongeza juhudi kupambana na hali kama hii, na kuwahamasisha wanasiasa kuacha kutoa kauli za kuchochea ubaguzi wa rangi, ili kulinda ipasavyo haki za binadamu za watu wote.