UM wasema fedha za misaada ya kibinadamu kwa mwaka 2021 nchini Somalia ni chache zaidi katika miaka 6 iliyopita
2021-07-15 09:13:48| CRI

Shirika la misaada la Umoja wa Mataifa limesema kuwa fedha zilizotolewa kwa ajili ya kuitikia mahitaji ya kibinadamu nchini Somalia ni chache zaidi katika miaka sita iliyopita.

Ofisi ya Uratibu wa Masuala ya Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa (OCHA) imesema kuwa mashirika ya kibinadamu hayajakidhi hata nusu ya mahitaji ya kimsingi ya watu wote wa Somalia.

Imeongeza kuwa uhaba wa fedha ni suala linalohitaji kufuatiliwa haraka, kwani hali ya zamani inaonyesha ukosefu mkubwa wa chakula nchini Somalia unaweza kuwa mbaya zaidi wakati wa misimu mingi ya ukame na kuweza kusababisha ukosefu mkubwa zaidi wa chakula endapo mvua hazitanyesha, kwa hivyo inahitaji kuongeza chakula, maji na mahitaji ya maisha ili kuzuia msukosuko.