Nchi 68 zaridhia taarifa ya pamoja kuiunga mkono China katika kikao cha 47 cha UNHRC
2021-07-15 09:12:26| CRI

Nchi zilizoridhia taarifa ya pamoja ya kuiunga mkono China kwenye kikao cha 47 cha Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa UNHRC zimefikia 68 baada ya Nigeria kufanya hivyo, kabla ya kumalizika kwa kikao hicho jana mjini Geneva, Uswisi.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Zhao Lijian amesema pamoja na nchi zilizoeleza kuunga mkono China kwenye hotuba zao na zile zilizowasilisha barua za pamoja, nchi zaidi ya 90 zimetetea haki kuhusiana na China kwenye UNHRC. Nchi hizo zimesisitiza kuwa masuala ya Hong Kong, Xinjiang na Tibet ni masuala ya ndani ya China ambayo hayapaswi kuingiliwa kati na nje. Pia zimekataa kufanya masuala ya haki za binadamu kuwa ya kisiasa na kutumia vigezo viwili pamoja na kupinga kuishutumu China bila ya msingi kwa malengo ya kisiasa.

Bw. Zhao amebainisha kuwa ukweli ukidhihiri daima uwongo hujitenga. Nchi chache za magharibi zimesambaza uwongo wa kisiasa na kuingilia kati masuala ya ndani ya nchi nyingine kwa kutumia kisingizio cha haki za binadamu kwenye UNHRC. Vitendo kama hivyo vimekuwa vikipingwa na vitaendelea kupingwa na jamii ya kimataifa.