Marekani kuorodheshwa nafasi ya kwanza duniani katika mapambano dhidi ya COVID-19 yaishushia heshima Bloomberg
2021-07-15 08:55:50| Cri

Katika sekta ya habari duniani, Shirika la habari la Marekani Bloomberg linajulikana kwa kutoa ripoti za kifedha duniani, na imekuwa ikijivunia kwa “kuwa na mtizamo usio na upendeleo na wa haki”. Lakini katika “Orodha za nchi zinazoshika nafasi za mwanzo dunani katika mapambano dhidi ya COVID-19” iliyotangazwa hivi karibuni na shirika hilo, Marekani imeorodheshwa kama ni nchi bora katika mapambano hayo, hali ambayo imestaajabisha dunia, na kulifanya shirika hilo lipoteze heshima.

Shirika la Bloomberg liliiwekea Marekani mfumo maalum wa tathmini, na kuifanya ishike nafasi ya mwanzo katika orodha hiyo, huku nchi na sehemu nyingine zinazotambuliwa kuwa na ufanisi mkubwa katika mapambano dhidi ya maambukizi ya virusi duniani zikiorodheshwa chini. Wakati orodha hii ilipotangazwa, baadhi ya watu walidhani ilikuwa imechapishwa vibaya.

Kwa nini Bloomberg inakiuka maadili ya kikazi na kuingia kwenye kashfa kama hii? Haishangazi baada ya kujua asili ya shirika hilo.

Kama tujuavyo, mwanzilishi wa Bloomberg ni meya wa zamani wa New York, ambaye pia ni bilionea Bloomberg. Kulingana na ripoti za vyombo vya habari, mwaka 2019 wakati Bloomberg alipotangaza ushiriki wake katika uchaguzi wa mwanzo wa urais ndani ya Chama cha Democratic, shirika hilo lilitangaza kuwa halitatoa tena ripoti za uchunguzi kuhusu Bloomberg na wagombea wengine wa urais wa chama hicho, lakini litaendelea na uchunguzi juu ya serikali ya Trump kutoka Chama cha Republican. Kutokana na hayo, upendeleo wa kisiasa wa shirika hilo ulionekana wazi.

Mwaka huu hatua ya shirika hilo vilevile imefichua asili yake ikiwa chombo cha kisiasa, nayo ni kuifurahisha serikali ya chama cha Democratic, na kutangaza mafanikio ya serikali ya chama hicho katika kupambana na maambukizi ya virusi. Lakini orodha iliyojaa uwongo haiwezi kuficha ukweli wa kushindwa kwa Marekani katika mapambano dhidi ya maambukizi ya virusi. Tangu kuibuka kwa janga hilo, zaidi ya watu laki sita nchini Marekani wamepoteza maisha. Idadi ya watu walioambukizwa na kufariki nchini humo kutokana COVID-19 imeshika nafasi ya kwanza duniani.