Wanadiplomasia wa nchi 48 wapinga kuufanya utafutaji wa chanzo cha COVID-19 kuwa wa kisiasa
2021-07-16 08:26:32| Cri

Wawakilishi wa kudumu wa nchi 48 katika Ofisi ya Umoja wa Mataifa huko Geneva UNOG wameongea na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus, wakieleza kuunga mkono kuhimiza utafutaji wa chanzo cha COVID-19 duniani, na kupinga kuufanya mchakato huo kuwa wa kisiasa.

Wanadiplomasia hao wamesisitiza kuwa COVID-19 ni adui wa binadamu, na itaweza tu kushindwa kwa mshikamano na ushirikiano wa jamii ya kimataifa.

Pia wamesisitiza kuwa utafutaji wa chanzo cha virusi ni suala la sayansi, na linapaswa kufanywa na wanasayansi kote duniani, lakini halipaswi kufanywa la kisiasa. Kama ushirikiano wa kimataifa katika mchakato huo utazuiliwa, juhudi za kupambana na janga la virusi duniani zitadhoofishwa.