China yatoa mwongozo wa mageuzi ya kiwango cha juu na ufunguaji mlango wa Pudong ya Shanghai
2021-07-16 08:26:09| Cri

China imetoa mwongozo wa kuunga mkono mageuzi ya kiwango cha juu na ufunguaji mlango wa eneo jipya la Pudong mjini Shanghai.

Mwongozo huo ulitolewa kwa pamoja na Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China na Baraza la Serikali, na kuorodhesha hatua za kuijenga Pudong kuwa eneo tangulizi kwa ujenzi wa kisasa wa ujamaa.

Kufuatia mwongozo huo, hadi kufikia mwaka 2035, Pudong itashuhudia ujenzi wake wa pande zote wa uchumi wa kisasa, maeneo ya kisasa yakijengwa, na utawala wa kisasa utatekelezwa kikamilifu. Kiwango cha maendeleo ya mji na uwezo wa ushindani wa kimataifa utaingia katika nafasi za mwanzo duniani.

Hadi kufikia mwaka 2050, Pudong inatarajiwa kuwa eneo muhimu litakalokuwa na mvuto, ubunifu, ushindani na ushawishi mkubwa duniani, ambalo litakuwa ni mfano mzuri wa utawala wa miji duniani.