Ubaguzi dhidi ya Waislamu ni tatizo sugu nchini Marekani
2021-07-18 17:57:06| CRI

Gazeti la Guangminribao la China limetoa tahariri, ikisema ubaguzi dhidi ya Waislamu ni tatizo sugu nchini Marekani.

Tahariri hiyo inasema Marekani inajidai kama “mnara wa kimataifa wa uhuru na demokrasia”, na “mlinzi wa haki za binadamu duniani”, lakini kwa muda mrefu inapuuza hali halisi ya ubaguzi dhidi ya Waislamu nchini humo, na kupuuza matakwa yao ya kuboresha maisha na kuwa na uhuru wa kuamini.

Ubaguzi dhidi ya Waislamu una historia ndefu nchini Marekani. Takwimu zinaonesha kuwa katika mwanzoni mwa karne 14, kati ya asilimia 10 na 15 ya watumwa wa Afrika nchini Marekani walikuwa wanaamini dini ya Kiislamu. Lakini walilazimishwa kubadilisha dini yao kuwa ya Kikristo. Baada ya kuingia kwenye karne ya 21, Marekani imekuwa na “hofu na Waislamu” mara kwa mara zaidi, na watu wengi waliopinga Uislamu nchini humo wameandika barua au kutoa maoni kwenye televisheni au mitandao ya kijamii, wakichochea uhasama dhidi ya Waislamu. Hata vyama vya Democratic na Republican vya nchi hiyo pia vinalichukulia suala la Waislamu kama njia ya kupata kura kwenye uchaguzi.