Waziri mkuu wa China atuma salamu za rambirambi kwa Chansela wa Ujerumani kufuatia mafuriko nchini humo
2021-07-18 17:59:23| CRI

Waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang tarehe 16 alituma salamu za rambirambi kwa Chansela wa Ujerumani Bibi Angela Dorothea Merkel kufuatia mafuriko makubwa yaliyotokea magharibi mwa nchi hiyo.

Kwenye salamu zake za rambirambi, Li amesema mafuriko makubwa yaliyotokea magharibi mwa Ujerumani yamesababisha vifo na majeruhi ya watu na hasara kubwa za mali. Akiwa kwa niaba ya serikali ya China, na yeye mwenyewe, ametoa salamu za rambirambi kwa wale waliokufa pamoja na familia zao. Anaamini kuwa chini ya uongozi wa Merkel, wananchi wa Ujerumani wanaweza kushinda maafa hayo na kujenga upya maskani yao.