Waziri wa mambo ya nje wa China kufanya ziara rasmi nchini Syria, Misri na Algeria
2021-07-18 17:59:59| CRI

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Zhao Lijian ametangaza kuwa, kwa mwaliko wa waziri wa mambo ya nje wa Syria Bw. Faisal Mekdad, waziri wa mambo ya nje wa Misri Bw. Sameh Shoukry na waziri wa mambo ya nje wa Algeria Bw. Ramtane Lamamra, waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi atafanya ziara rasmi katika nchi hizo tatu kuanzia tarehe 17 hadi 20 mwezi Julai.