Hotuba ya rais Xi Jinping katika Mkutano wa Maadhimisho ya Miaka 100 tangu kuanzishwa kwa CPC yachapishwa kwa lugha mbalimbali
2021-07-20 19:00:41| CRI

Hotuba ya rais Xi Jinping wa China katika Mkutano wa Maadhimisho ya Miaka 100 tangu kuanzishwa kwa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) ambayo ilitafsiriwa na Taasisi ya Utafiti wa Historia ya CPC na nyaraka kuhusu Kamati Kuu ya chama hicho, hivi karibuni imechapishwa na Shirika la Uchapishaji la Serikali Kuu kwa lugha sita zikiwemo Kirusi, Kifaransa, Kihispania, Kiarabu, Kijapani, na Kijerumani. 

Hotuba hiyo ya rais Xi imekumbuka mafanikio makubwa yaliyofanywa na watu wa makabila mbalimbali kote nchini China wakiongozwa na CPC katika miaka 100 iliyopita tangu kuanzishwa kwa chama hicho. Kuchapishwa kwa hotuba hiyo kuna umuhimu mkubwa katika kuwasaidia wasomaji wa nchini na nje ya nchi kuelewa zaidi historia na mafanikio makubwa ya CPC ya kuongoza Wachina kufanya juhudi bila ya kusita, na kuenzi thamani ya pamoja ya binadamu ya amani, maendeleo, haki, demokrasia na uhuru.