Mke wa rais wa China atoa hotuba kwa njia ya video kwa mkutano wa baraza la elimu na kupunguza umaskini la wanawake la shirika la SCO
2021-07-20 16:47:36| CRI

Mke wa rais wa China ambaye pia ni balozi wa kuhimiza elimu za wasichana na wanawake wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa UNESCO Bibi Peng Liyuan ametoa hotuba ya video kwa mkutano wa baraza la elimu na kupunguza umaskini la Jumuiya ya ushirikiano ya Shanghai SCO.

Bibi Peng amesema, kuondokana na umaskini na kukumbatia maisha bora ni ndoto ya pamoja ya wanawake wote. Wanawake wanaweza kupata nguvu ya kuondoa umaskini kupitia kupata elimu, ujuzi na ufundi. Kupitia juhudi kubwa, China imepata ushindi wa pamoja katika vita dhidi ya umaskini, huku wanawake wa China wakiondokana kabisa na umaskini. Tumechukua hatua za mfululizo kuhakikisha wanawake wana haki za kupata elimu, kuwawezesha kuwa washiriki, wachangiaji na wanaonufaika na ushindi wa vita dhidi ya umaskini.

Pia amesema,  kutilia maanani kwa serikali, kuunga mkono kwa mashirika ya kijamii na mchango wa watu kutoka hali mbalimbali zimetoa nguvu ya kuhimiza shughuli ya kutoa elimu na kupunguza umaskini kwa wanawake.

Peng ameongeza kuwa hivi sasa wanawake milioni 435 kote duniani wanaishi katika hali ya umaskini, pengo la kijinsia katika upatikanaji wa elimu bado ni kubwa, huku maambukizi ya COVID-19 yakileta changamoto mpya kwa wanawake.