Watu wasiopungua 28 wauawa kwenye mlipuko wa mabomu mjini Baghdad
2021-07-20 09:18:39| cri

Watu wasiopungua 28 wameuawa na wengine 66 wamejeruhiwa kwenye mlipuko mmoja wa mabomu dhidi ya soko moja maarufu huko Sadr kwenye kitongoji cha Baghdad nchini Iraq. Mlipuko huo pia umeharibu maduka kadhaa na majengo karibu na soko hilo. Huku mamlaka husika za Iraq zimesema habari zaidi kuhusu mlipuko huo zitatolewa baada ya uchunguzi kukamilika.

Milipuko mikubwa wa mabomu umekuwa nadra huko Baghdad kutokana na hali ya usalama nchini Iraq kuboreshwa tangu jeshi lake kuwashinda wapiganaji wa kundi la IS mwaka wa 2017. Wapiganaji waliobaki wa kundi hilo wamejificha kwenye sehemu mbalimbali za nchi hiyo na kufanya mashambulizi ya kuvizia dhidi ya majeshi ya serikali na raia nchini humo.